kampala international universty

Friday, 23 March 2018

NATIONAL ID REGSTRATION FORM

Kindly find the easiest way to register your name for national id. Through the announcement released today early by the Kampala students union organisation KIUTSO



For registration click on the link below.

UFAHAMU VIZURI UGONJWA WA HOMA YA INI



HOMA YA INI (HEPATITIS)  NI NINI ??
Nimekuwa nikipokea maswali mengi saana kuhusiana na ugonjwa huu wa homa ya ini. Na hii inaonesha ni jinsi gani watu wengi walivyo na Kiu na hamu ya kuujua kwa undani ugonjwa huu wa homa ya ini.
Kwa tafiti chache zilizofanyika mpaka sasa imegundulika kuwa kati ya watu 117 ni mtu 1 tu anakuwa ameathirika na virusi vya UKIMWI/VVU  lakini ni watu 22 wanakuwa wameathirika na HOMA YA INI sawa na asilimia  18.8%  lakini pia vifo vinavyosababishwa na homa ya ini kwa report ya dunia mpaka sasa ni mil 1.35  kwa mwaka.
Maambukizi ya HOMA YA INI yameongezeka kutoka milion 1.1 mpaka milion 1.7 kwa mwaka tofauti kabisa na maambukizi ya VVU/ UKIMWI  ambayo ni mil 1.3 kwa mwaka hivyo hapa tunaona ni jinsi gani ugonjwa huu unazidi kusambaa kwa kasi zaidi.
Report ya wizara ya afya nchini iliyosomwa na waziri wa afya. July mwaka 2017 kuhusiana na homa ya ini inaonyesha kuwa katika watanzia 100 ni watanzia 8 hupata maambukizi sugu ya ugonjwa huu ( chronic hepatitis). Hivyo basi kati ya watanzia million 55 ni watanzania mil 4.2 wanapatwa na ugonjwa sugu wa homa ya ini
Ndugu zangu ugonjwa wa homa ya ini ni ugonjwa hatari saana si tu kwamba unasababisha vifo taratibu au kimya kimya lakini ugonjwa huu unapoupata haujuchukui muda mrefu mpaka kufikia  kifo lakini pia njia za ugonjwa huu kusambaa ni rahisi mno ukilinganisha na magonjwa mengine kama virusi vya UKIMWI
Sambamba na hilo kirusi wa homa ya ini ni kirusi ambae ni hatari zaidi kwani anasifa ya pekee ambayo anauwezo wa kukaa nje ya damu kwa muda wa siku zisizo pungua 7 na kusababisha maambukizi  ya ugonjwa kwa mtu mwingine hii ina maana kwamba *iwapo ulitumia taulo la mtu aliyeathirika na virusi hivi ndani ya siku saba unakuwa katika mazingira rahisi zaidi ya kuambukizwa* hii ni tofauti kabisa na virusi vya VVU/UKIMWI ambapo kirusi wa VVU/UKIMWI hana uwezo wa kukaa nje ya damu hata dakika 1.
HOMA YA INI.
ni ugonjwa ambao mtu anaupata baada ya kuambukizwa na kirusi aina ya HBV au HCV ambavyo hushambulia INI na kusababisha *KANSA YA INI .* Kuna aina 5 ya homa ya ini ambayo ni homa ya ini A, B, C, D, na E. . Watu wengi saana hupata maambukizi ya homa ya ini B na watu wenye virusi vya UKIMWI huambukizwa kwa urahisi zaidi na homa ya ini C . Virusi hivi vinapoingia ndani ya mwili huchukua siku 45 mpaka siku 90 kukomaa . Na ndani ya siku 60 mtu anapopimwa homa ya ini tayari huwa inajionyesha kuwepo ndani ya mwili
Virusi hivi vinapozaliana kwa wingi ndani ya ini hubadilisha mfumo wa kawaida wa ufanyaji kazi wa ini na kupelekea mtu kupata KANSA YA INI. Ambayo hii sasa ndo husababisha kifo kwa watu wengi.
  NJIA ZA MAAMBUKIZI
Homa ya ini huambukizwa kwa kugusana na Maji maji / vimiminika Vyovyote vile kutoka kwa mtu aliyeathirika na ugonjwa huu. Vimiminika hivi ni kama
1. Damu
2. Mate
3. Jasho
4. Kuchangia vitu vyenye ncha kali
6. Maji maji ya sehemu za siri
7 kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto
Watu waliokatika mazingira hatarishi zaidi ambayo ni rahisi zaidi kupata ugonjwa huu ni
1. Wauguzi wa AFYA
2. Watumiaji wa pombe kupita kiasi (ULEVI)
3.Matumizi mabaya ya Dawa  ikiwemo DAWA ZA KULEVYA
4. Waathirika wa virusi ya UKIMWI/VVU. Na magojwa yapunguzayo kinga za mwili.
5. kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto
Tafiti zinaonesha kuwa watoto wanaozaliwa na homa ya ini wengi wao hukuwa nayo na kupelekea kufikia hatua za kuwa ugonjwa sugu ndani ya mwili wao na hatimaye kifo
DALILI ZA UGONJWA HUU
HOMA YA INI kwa watu wengi haionyeshi dalili za awali pale tu mtu anapoambukizwa ni watu wachache saana ambao  huonyesha dalili za awali za ugonjwa huu ambazo ni
Uchovu kila mara, homa wakati wa jioni , kutokwa jasho jingi wakati wa usiku
Ugonjwa huu mara nyingi na kwa watu wengi huonyesha dalili zake unapokuwa umefikia hatua za mwisho yaani unapoona dalili basi ujue KIFO KIPO KARIBU  dalili hizo ni
1. Homa
2. Uchovu muda wote
3. Macho kuwa ya njano
4. Maumivi makali yafuatanayo na uvimbe sehemu ya juu kulia kwa tumbo
5. Kutapika damu
6. Ngozi kubadilika
7 kutokwa damu bila kujizuia unapoumia
8. Kutokwa na damu kwenye fizi
MATIBABU
HOMA YA INI  mpaka sasa haina dawa rasimi za kuondoa ugonjwa huu lakini  uzuri ni kwamba ugonjwa huu una CHANJO  ambayo inazuia maambukizi ya ugonjwa huu. Chanjo hii hutolewa kwa sindano 3 ndani ya kipindi cha miezi 8 . Ambapo sindano ya kwanza (1)  hutolewa  ikifuatia sindano ya pili (2) ambayo hutolewa mwezi mmoja baada ya sindano ya kwanza na ya tatu (3) baada ya MIEZI 6
CHANJO hii hutolewa kote nchini lakini pia kwa kutambua umuhimu wa suala hili serikali imeanzisha kitengo maalumu cha clinic katika hospitali ya TAIFA  MUHIMBILI ambapo hushughulika na ugonjwa huh wa HOMA YA INI
lakini pia unapogundulika na ugonjwa huu mapema unapewa dawa za kuweza kupunguza kiwango cha wadudu (virusi) kuzaliana kwa wingi na kusababisha KANSA YA INI na hatimaye kupelekea kifo
Hivyo kupima mapema kunakufanya wewe kujijua mapema na kuanza kupokea matibabu mapema
Jali afya yako, pima afya yako .
Dr FROLIAN MWEBESA
+255 762 55 45 85 / + 255 719 55 21 71
Facebook: dr frolian mwebesa
Instagram: drfrolianmwebesa